Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mb) ametaka viwanda vyote nchini kutengeneza  bidhaa zenye ubora  kwa gharama nafuu  ili ziweze kuingia katika soko  Eneo huru la biashara Afrika (AfCFTA)

Waziri Kijaji ameyasema hayo Agosti 3, 2023 alipotembea Kiwanda cha kuzalisha Maziwa cha Tanga Fresh kilichopo jijini Tanga kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji  wa maziwa  na kusikiliza na kutatua changamoto walizonazo. 

Aidha amebainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inafanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha wafanyabiashara na wawekezaji  wanakuwa na mazingira bora na wezeshi ili kufanya biashara kwa tija na kukuza uchumi wa Taifa. 

Vilevile  amesema  Serikali ya Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Tanzania nikuona wafugaji wanabadilika kutoka katika ufugaji wa kienyeji kwenda  katika uwekezaji  wa kisasa  ili  kukidhi mahitaji ya soko.

Aidha amepongeza kiwanda hicho kwa ajira walizotoa hapa nchini na ametaka  ajirasizizo za moja kwa moja  ziongezeke.