Habari
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Ashatu Kijaji(Mb.) ameushauri uongozi wa Mkoa wa Tanga kushirikiana na Taasisi husika kutatua changamoto

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Ashatu Kijaji(Mb.) ameushauri uongozi wa Mkoa wa Tanga kushirikiana na Taasisi husika kutatua changamoto za wanazopata wafanyabiashara wa Jiji la Tanga.
Dkt. Kijaji ameyasema hayo Agosti, 3 2023 alipokua na wafanyabiashara Jijini Tanga kwa lengo la kusikiliza changamoto zao za kibiashara na kuzitafutia ufumbuzi.
Aidha, amebainisha kuwa Dhamira ya Serikali nikulirudisha jiji la Tanga kuwa jiji la Viwanda nchini kama hapo awali ili liweze kutoa ajira kwa vijana kukuza biashara na uchumi wa Taifa .
Vilevile, amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rai wa Jmhuri ya Muungano wa Tnzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeamuaa kukabidhi uchumi katika sekta binafsi ili uchumi uwe imara ndani na nje ya Nchi.
Dkt. Kijaji pia ameishauri TRA isiwabebeshe mzigo wafanyabiashara kwa kulimbikiza kodi bali ameitaka TRA ishirikiane na wafanyabiashara hao na kiwapa elimi kuhusu ulipaji kodi ili kukuza uchumi.