Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo ametoa rai kwa wawekezaji nchini kuongeza wigo wa uwekezaji ili kuendeleza uchumi wa Viwanda ndani ya nchi.


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo ametoa rai kwa wawekezaji nchini kuongeza wigo wa uwekezaji ili kuendeleza uchumi wa Viwanda ndani ya nchi.

Amesema wamiliki wa Viwanda wana haja kubwa ya kuitana Nchini pamoja na kuongeza wigo wa uwekezaji wa Viwanda kwenye maeneo mbalimbali yaliyopo nchini.

Dkt.Jafo ametoa rai hiyo alipotembelea Kiwanda cha Vioo cha KEDA kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani Disemba 03,2024.

Aidha Waziri Jafo ameridhishwa na shughuli za uzalishaji zinazofanywa na Kiwanda hicho ambacho kina soko kubwa la vioo ndani na nje ya Nchi ya Tanzania kuwa moja ya Kiwanda kilichotoa ajira kwa watu 800 ambapo ni matumaini yake mpaka kukamilika kwa kiwanda hicho kutaweza kutoa ajira zaidi ya watu 3000 ambapo itakuwa fursa kwa Watanzania na Taifa kwa ujumla.

Amesema Wizara ipo katika kusaidia malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ya uwekezaji wa Viwanda nchini yanatimia na ndio maana Wizara imekuja na Mpango wa ujenzi wa Viwanda wa Miaka Sita katika Mikoa na Wilaya zote Nchini.

Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkuranga Bw.Omary Mwanga akizungumza kwaniaba ya Mkuu wa Wilaya amesema uwekezaji wa Kiwanda hicho umekuwa msaada mkubwa kwenye ajira kwa vijana,Mapato ya Serikali lakini pia kushirikiana kwenye mambo ya kijamii.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Bw.Tony Wu amesema malengo ya kiwanda hicho ni kuwa kiwanda ambacho kinazalisha kioo bora ambacho kitaweza kutumika ndani na nje ya nchi ya Tanzania.