Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo amekutana na kufanya kikao na wadau mbalimbali wa usafirishaji, uingizaji na utoaji wa mizigo bandarini. 


Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo amekutana na kufanya kikao na wadau mbalimbali wa usafirishaji, uingizaji na utoaji wa mizigo bandarini. 

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kililenga kujadili kwa pamoja changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wadau hao ambazo zimekuwa zikiathiri mazingira na hali ya biashara hapa nchini. 

Aidha, kikao hicho kilitumika kupokea maoni mbalimbali kutoka kwa wadau hao kuhusu utendaji wa majukumu yanayofanywa na Shirika la Viwango Tanzania TBS katika Bandari ya Dar es Salaam, hususan jukumu jipya la ukaguzi wa magari yanayoingizwa nchini.

Kikao hicho kimefanyika Leo Mei 03, 2021katika ukumbi wa Mikutano wa Bandari ya Dar es salaam na  kimehudhuriwa na wadau mbalimbali na wawakirishi wa Taasisi za TAFFA- Tanzania freight forwarding Association, TATOA- Tanzania Truck Owners Association, TASAA- Tanzania Shipping agency's Association, CIDAT- Container Inland Deports  Associations of Tanzania, TSC- Tanzania Shippers Council, TICTS- Tanzania International Container Terminal Services.