Habari
TUWAJIBIKE KUIMARISHA UTENDAJI KAZI WA TAASISI-MBWASI.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Aristides Mbwasi amewataka Watumishi wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) kufanya kazi kwa ushirikiano na uwajibikaji ili kuendelea kuimarisha utendaji wa taasisi pamoja na huduma zinazotolewa kwa wadau wake.
Amebainisha hayo wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Bodi hiyo Mei 8, 2026, katika Ukumbi wa Edema mkoani Morogoro.
Aidha katika Kikao hicho cha Baraza kimejadili Bajeti ya mwaka 2026/2027 pamoja na kujadili namna bora ya kutatua kero mbalimbali za watumishi mahali pa kazi ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa WRRB Bw.Asangye Bangu amesema Mfumo wa Stakabadhi za ghala umekuwa chachu ya mabadiliko katika uzalishaji wa bidhaa na umedhihirisha katika mazao mbalimbali ikiwemo korosho, kakao, kahawa na choroko pamoja na ongezeko la bei.
Aidha amesema Mifumo ya tehama imwkuwa chagizo kuwezesha taasisi kufikia mafanikio hasa kwa kuweka mifumo imara ya kusimamia mazao.
