Habari
Zaidi ya kampuni 150 kutoka China kuwekeza nchini.
Waziri wa viwanda na biashara Dk. Seleman Jafo amesema kupitia maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa takribani kampuni 150 kutoka China zimeonesha nia ya kuwekeza nchini.
Ameyasema hayo Julai 13 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya ufungaji Maonesho hayo yaliyoanza Juni 28,2024 hadi Julai 13, 2024.
“Kampuni nyingi kutoka nje zimekutana na wafanyabiashara wa hapa nchini na kutoa fursa kwa kutumia masoko ya nje ya nchi kupeleka bidhaa zao. hivyo Maonesho ya Sabasaba yanaipa fursa Tanzania kushiriki katika maonesho katika nchi mbalimbali. Amesema Dkt Jafo
Akifafanua zaidi kuhusu kauli mbiu ya maonesho hayo ambayo Tanzania ni Mahali Salama kwa Biashara na Uwekezaji” Dkt Jafo amebainisha kuwa na kuna fursa mbalimbali za ufanyaji biashara na uwekeaji Tanzania bara na visiwani
Aidha Dkt. Jafo amewakumbusha wafanyabiashara nchini kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi.