Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo Mhe. Deodatus Mwanyika (Mwenye kofia) akiongozana na wajumbe wa kamati hiyo baada ya kuwasili kwenye kituo cha 'train' ya mwendokasi (SGR) cha Dar Es Salaam kutokea Dodoma kwa ajili ya ziara ya Kamati hiyo ya kutembelea, kuona na kujifunza utekelezaji wa shughuli za Kiwanda cha Lodhia kilichopo Mkuranga (Pwani) Februari 8, 2025.