Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Dkt. Hashil Abdallah (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda wa Zambia, Bi. Lilian Bwalya wakisaini makubaliano


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara na Viwanda wa Zambia, Bi. Lilian Bwalya wakisaini makubaliano ya kurahisisha mazingira ya kibiashara kati ya Tanzania na Zambia.
Makubaliano hayo ni baada ya Mkutano wa Nne (4) wa Kamati ya Pamoja ya Biashara (Joint Trade Commitie-JTC) kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zambia ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika Agosti 20, 2025 Nakonde Zambia.

Mkutano huo ngazi ya Makatibu Wakuu ulitanguliwa na Mkutano wa Watalaam uliofanyika Agosti 18 na 19, 2025 Nakonde, Zambia.