VIWANDA 80,000 VYATOA AJIRA MILIONI TANO
MIAKA MINNE YA RAIS SAMIA,WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YATOA AJIRA MILIONI TANO KWA WATANZANIA
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Dkt. Selmani Jafo(Mb) amesema Takwimu zinaonesha kwa sasa kuna Viwanda zaidi ya 80,000 ambavyo vimetoa ajira kwa zaidi ya watanzania milioni 5.
Kauli hiyo ameitoa Mei 15,2025 Jijini Dodoma wakati akieleza mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya Sita.
Waziri Jafo amesema Takwimu zinaonesha kwa sasa kuna Viwanda 80,000 ambavyo vingi ni vidogo ambavyo vimetoa ajira zaidi ya milioni tano.
Aidha,amesema Serikali inakuja na Mpango wa sensa ya Viwanda ambao utaanzia Mkoani Mwanza na Shinyanga lengo likiwa ni kuhakikisha inapata idadi ya Viwanda,vikubwa vya kati na vidogo
Vilevile,Waziri Jafo amemshukuru Rais Samia kwa kufungua fursa za Biashara na uwepo wa Viwanda vingi nchini.