Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

SERIKALI HAIPO TAYARI KUONA UJUZI WA VIJANA UNATOWEKA- LONDO


Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema haipo tayari kuona ujuzi wa vijana nchini unatoweka kwa kuhakikisha inaweka mifumo thabiti katika kukuza juzi zao.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo (mb) wakati wa Ufunguzi rasmi wa Kongamano la Kitaifa kuhusu nafasi ya vituo vya ubunifu na kongani za viwanda katika kuendeleza jasiriamali ndogo na za kati (SMEs) nchini Tanzania linayofanyika Cate Hotel Mkoani Morogoro Julai 20,2026.

Mhe. Londo amesema kama Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya biashara kupitia mageuzi ya sera, sheria na kanuni ili kuounguza urasimu na gharama za kufanya biashara pamoja na kuimarisha upatikanaji wa fedha kupitia ushirikiano wa tassisi za fedha.

Aidha Londo amesema lengo la Serikali ni kuhimiza uanzishwaji wa vituo vya ubunifu na kongani za viwanda (hub & clusters) kwenye sekta zenye fursa pamoja na kuzifanya kuwa hazibaki kuwa maeneo ya mafunzo pekee balikuwa vituo vya kuzalisha biashara zinazokua, kutoa ajira, kuongeza mauzo ya nje na kuchangia pato la Taifa.

Vilevile Londo ametoa wito kwa wadau walioshiriki Kongamano hilo kama fursa ya kujenga makubaliano yatakayowezesha Tanzania kuwa na mfumo jumuishi wa kusaidia jasiriamali ndogo na za kati, mapendekezo yanayotekelezeka, yanayojenga ushirikiano baina ya Serikali, Sekta binafsi na taasisi za elimu,tafiti, fedha na washirika wa maendeleo.