Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

BALOZI SALUM AAGIZA WAWEKEZAJI KUTOA KIPAUMBELE AJIRA ZA WAZAWA


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Balozi Waziri Salum, amewataka wawekezaji wanaowekeza katika sekta ya viwanda nchini kuhakikisha wanatoa kipaumbele cha ajira kwa wazawa ili waweze kunufaika na uwekezaji huo.

Balozi Salum ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kutembelea viwanda mbalimbali katika Jiji la Tanga, Aprili 24, 2026 ikiwemo kiwanda cha Nellkanth Chemicals na Tanga Cement. Amesema lengo la ziara hiyo ni kujifunza, kufahamu hali ya sekta ya viwanda na biashara pamoja na ajira viwandani kwa Mkoa wa Tanga, pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili wawekezaji wa Viwanda hivyo.

Aidha Balozi Salum amewasisitiza wawekezaji wa Viwanda kuhakikisha suala la ajira kwa wazawa linapewa kipaumbele. Aidha, wanawake nao waangaliwe kwa karibu kwani wana uwezo mkubwa na wanaweza kufanya kazi yoyote.

Vilevile Balozi Waziri amewahakikishia wawekezaji wote nchini kuwa Wizara ya Viwanda na Biashara itahakikisha inaendelea kuwaweka karibu wawekezaji hao na kuwapatia ushirikiano wa karibu ili kuweka mazingira rafik kwao.

Nae Meneja wa uzalishaji wa Kiwanda cha Tanga Cement Bw. Gadiel Munuo ameishukuru Serikali kwa kuwawekea mazingira wezeshi hasa kwenye bidhaa ya sari inayozalishwa kwani bidhaa hiyo inakwenda sokoni kwa wingii zaidi tofauti na kipindi cha nje walizokuwa wanapambana na bidhaa za nje.