Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Baraza Hakikisheni malengo ya TIRDO na TAIFA Yanafikiwa


Naibu  Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb.) ameliagiza Baraza la Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) kuandaa mkakati  ya utekelezaji wa mipango ya Shirika ili kuhakikisha malengo ya Taifa, Wizara na TIRDO yanafanikiwa.

Kigahe ameyasema hayo katika hafla fupi ya uzinduzi wa Baraza hilo iliyofanyika Septemba 28, 2022 jijini Dar es Salaam  ambapo Baraza hilo  na Menejimenti litapimwa kwa kutumia mkataba wa utendaji kazi (Perfomance Contract) utakaosainiwa kati yao na Msajili wa Hazina.

Aidha, Kigahe ameliagiza Baraza hilo kutoa ushauri sahihi unaolenga kuleta tija kwa shirika nankutatua  kutatua changamoto za shirika, kuleta mawazo mapya ya kuboresha uendeshaji wa shirika na  utoaji wa huduma mpya zitakazoimarisha utendaji  kazi na utatuaji wa migogoro wakati wa utekelezaji wa majukumu.

Kigahe amewaeleza wajumbe wa Baraza  hilo  kuwa watunza nidhamu wa Menejimenti na watumishi wa Shirika hilo kwa niaba ya Serikali ili  kuhakikisha  Menejimenti inatekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za nchi.

“Nimeona vile vile, bunifu mbalimbali ambazo zimelenga kuleta suluhisho kwa Watanzania kwa kusaidia teknolojia rahisi za kuongeza thamani ya mazao na hivyo kuwezesha uanzishwaji wa viwanda vidogo na vya kati,” ameongeza Kigahe.

Vilevile,  ametoa rai kwa Baraza hilo na Mejimenti, kuendelea kuandika maandiko mbalimbali (project proposals) kwenda kwa wadau mbalimbali wa kisekta ili kupata fedha za utafiti na kubuni teknolojia rahisi  ambazo zitaendelea kuwasaidia wakulima, wavuvi, wafugaji na sekta zingine zote zinazotoa ajira kupitia viwanda