Habari
BRELA Yatakiwa Kutatua Changamoto za Leseni na Usajili

Kamati ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira imeipongeza BRELA kwa kazi nzuri na kuiagiza BRELA, EPZA na TIC zilizo chini ya Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara zinahusika na utoaji wa Leseni au vibali kufanya kazi kwa pamoja ili kuwa na takwimu sahihi za Wafanyabiashara Nchini.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. David Kihenzile (Mb) wakati wa kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa jukumu la Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni la Usajili wa Kampuni oktoba 25 Bungeni Dodoma.
Naye Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akijumuisha maoni na mapendekezo ya Kamati hiyo ametoa agizo kwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kutokufunga Biashara na badala yake kukaa a Wafanyabiashara na kutatua Changamoto walizonazo katika masuala ya Leseni na Usajili wa Makampuni ili kuboresha Mazin[1]gira ya Biashara.
Mhe. Dkt. Kijaji ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuweka Mazingira ya Biashara kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na uwekezaji (MKUMBI) na ameitaka BRELA kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu Usajili wa Makampuni, Leseni na Umiliki Manufaa.
Nao Wajumbe wa Kamati hiyo walitoa maoni na mapendekezo mbalimbali yanayolenga kuboresha huduma za BRELA ikiwemo Uhuishaji wa taarifa, uhusiano wa biashara kati ya Tanzania Bara na Zanzibar, Umiliki Manufaa na Sheria ya Leseni na usajili wa viwanda ya mwaka 1967 ambayo ina uhitaji mkubwa wa kuhuishwa.
Akijibu baadhi ya maswali ya Wajumbe wa Kamati hiyo Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Bw. Godfrey Nyaisa amesema kuwa BRELA imeendelea kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika utoaji wa huduma na kutumia mifumo ya Kielektroniki ya Utoaji Huduma za Sajili (ORS) na Utoaji wa Leseni za Biashara (NBP).
Awali akiwasilisha taarifa ya usajili wa Makampuni pamoja na jukumu la utoaji Leseni Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Makampuni BRELA Bi. Leticia Zavu amesema kuwa BRELA imekuwa ikitoa elimu ya mara kwa mara kupitia vyombo mbalimbali vya habari kwa waliosajili kampuni, kampeni juu ya matumizi ya mifumo ya TEHAMA na ukaguzi elimishi kwa kuwatembelea Wafanyabiashara kuwasikiliza na kutatua changamoto wanazopa