Habari
(CAMARTEC) kuleta mabadiliko zaidi katika uzalishaji na udhibiti wa zana za kilimo
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt.Selemani Jafo ameiagiza Bodi ya Wakurugenzi wa Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini (CAMARTEC) kuleta mabadiliko zaidi katika uzalishaji na udhibiti wa zana za kilimo zinazoingia kutoka nje ya nchi ikiwemo kutopata hati chafu sanjari na matumizi sahihi ya fedha.
Waziri Jafo ameyasema hayo Januari 24, 2025 wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa CAMARTEC, Jijini Arusha ambapo Mwenyekiti wa Bodi hiyo kula kiapo cha Maadili.
Alisisitiza Bodi hiyo kusimamia vema kazi za kituo hicho ikiwemo kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili kuhakikisha zana za kilimo zinawafikia wananchi wengi hususani wakulima ili waweze kuwa na matumizi sahihi ya zana za kilimo na vema ili kuhakikisha CAMARTEC inapata maendeleo.
Vilevile Dkt Jafo ameishauri Bodi hiyo kuendelea kutoa ushauri ikiwemo kusimamia Menejinenti na Wajumbe wake kufanya kazi kwa upendo na nidhamu kazini ili kuhakikisha wanaleta tija katika kituo hicho ili kuhakikisha wanatoa matunda bora.
Vilevike Dkt Jafo ameziagiza Taasisi zote zilizochini ya Wizara yake ikiwemo CAMARTEC kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya Kitengo cha Habari na Mawasiliano ili kiweze kutejeleza majukumu yake ipasavyo katika kuelimisha umma kuhusu jitihada mbalimbali za kuendeleza sekta ya viwanda na biashara.
Naye Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Needpeace Wambuya akimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara,Dkt,Hashil Abdalah amesema anaamini Bodi hiyo itasimamia kwa ukamilifu tafiti na majaribio ya teknolojia kwa ajili ya zana za kilimo zinazoingizwa nchini kutoka nje ya nchini
Akisoma taarifa ya kituo hicho, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa CAMARTEC, Injinia Godfrey Mwinama amesema Kituo hicho kimefanikiwa kuunda zana mpya 42 zinazozalisha zana mbalimbali kwa ajili ya kuongeza tija katika kilimo
Awali Mwenyekiti wa Bodi ya CAMARTEC, Profesa Valerian Silayo alisema Bodi hiyo imepokea maelekezo yote yaliyitolewa na iko tayari kuyafanyia kazi ili kuhakikisha CAMARTEC inafikia malengo yaliyokusudiwa ikiwemo kusaidiwa upatikanaji wa fedha za kuendesha kituo hicho kwa wakati