Habari
CAMARTEC ongezeni ubunifu wa kuzalisha zana za kilimo zinazowasaidia wakulima kwa wingi ili kukidhi mahitaji

Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji Mei 28, 2022 amekitaka Kituo cha Uzalishaji zana za Kilimo Vijijini (CAMARTEC) kuongeza ubunifu na kuzalisha zana za kilimo zinazowasaidia wakulima kwa wingi ili kukidhi mahitaji ya zana hizo nchini na kuongeza tija katika kilimo kwa kushirikiana na Taasisi nyingine kama SIDO,TIRDO,TEMDO na nyingine zinazohusika ili kuongeza ufanisi katika uzalishaji wa zana hizo.