Habari
CBE Boresheni wa mitaala ya kozi ili ziendane na mahitaji ya Soko la Ajira

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah Februari 13, 2023 amekutana na kujadiliana na Menejimenti ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kuhusu uboreshaji wa mitaala ya kozi zinazotolewa na chuo hicho ili iendane na mahitaji ya soko la ajira na mabadiliko ya teknolojia pamoja na kifanya utafiti unaolenga kutatua changamoto mbalimbali katika jamii na kukuza biashara nchini.