Habari
CBE YAPANDA NAFASI YA UBORA WA VYUO VIKUU KUTOKA NAFASI YA 54 HADI 14
Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo apongeza Chuo Cha Elimu ya Biashara (CBE) kwa kupanda kwenye ubora wa vyuo vikuu (University Webometric ranking) kutoka nafasi ya 53 hadi ya nafasi ya 14 hapa nchini.
Prof. Mkumbo alitoa pongezi hizo wakati alipokuwa Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 56 ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kamapasi ya Dar es salaam yaliyofanyika Novemba 13, 2021
“Chuo Cha Elimu ya Biashara kwa muda mrefu kilikuwa ni Chuo ambacho kinajulikana kuwa ni chuo kizuri lakini katika ngazi ya kitaaluma kilikuwa mbali sana, sasa nipongeze kwa kupanda kwenye ubora wa vyuo vikuu nchini kutoka nafasi ya 53 hadi nafasi ya 14” alieleza Prof. Mkumbo
Prof. Mkumbo aliupongeza Uongozi wa Chuo kwa kwa kufanikisha mipango yake mbalimbali ambayo ni kutumia vizuri fedha za ndani kukarabati jengo la Cafeteria katika kampasi ya Dar es salaam ambalo tayali limekamilika, maendeleo mazuri ya mradi mkubwa wa ujenzi wa hosteli za wanafunzi na kukabidhiwa eneo la Chwaka, Zanzibar kwa ajiri ya kuanzisha tawi jingine.
Aidha, Prof. Mkumbo alisema kuwa takwimu zinaonesha kuwa kuna ukosefu wa fursa za ajira hasa kwa vijana ambapo takribani asilimia 10.4 ya watanzani hawana ajira wakati huo kila mwaka vijana takribani 800, 000 wanahitimu masomo yako, hivyo njia pekee ya suluhisho hilo ni kujiajiri kupitia ujasiriamali.
Prof. Mkumbo wakati akieleza umuhimu wa masomo ya ujasiliamari na hali ya ujasiriamali nchini alibainisha kuwa ujasiliamari ni pamoja na kuendeleza vipaji tulivyonavyo vilevile uwezo wa kufikiri na kupambanua mambo muhimu kwa mafaniko ya mtu mmoja katika ulimwengu wa biashara hivyo elimu ya ujasirimali inahitajika sana nchini ili kuzitumia kwa ufanisi fursa na rasilimali zilizopo.
Vilevile, Prof. Mkumbo alisema kuwa Serikali inaendelea kudumisha ushirikiano wa kimataifa na nchi za Jirani kupitia Jumiya ya Afrika Mahariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika (SADC) na sasa Tanzania imejiunga na Mkataba wa eneo huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA).
Pia, Prof. Mkumbo alitoa ushauri kwa wahitimu kwa kuwataka kujikita kutafuta nafasi kazi kuliko ajira kwa sababu ajira ni chache lakini kazi zipo nyingi, pia aliwahasa kuheshimu matakwa yao kwa kufanya vitu wanavyoamini ni sahihi na vizuri vitakayoyotambulisha utu wao, vilevile kuwa sehemu ya jamii kwa kufanya mambo kwa kushirikiana.
Kwa Upande Wake Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara, Prof. Emmanuel Mjema alieleza kuwa katika kipindi chote za miaka 56, Chuo kimetoa mchango mkubwa katika Taifa letu kwa kuzalisha wataalam wabobezi katika fani za biashara kwa kutoa elimu, kufanya tafiti mbalimbali na kutoa ushauri wa kitaalam katika nyanja za biashara, uchumi, uongozi, teknologia ya habari, manunuzi, ugavi pamoja na vipimo na viwango
Nae, Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi ya Chuo cha Elimu ya Biashara, Prof. Wineaster Anderson alisema kupitia majukumu matatu ya makuu ya Chuo cha CBE ambayo ni kutoa mafunzo katika tasnia ya biashara, kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu, Chuo kinaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kujenga uchumi shidani na viwanda kwa maendeleo ya watu zilizoainishwa kwenye mipango ya maendeleo ya Taifa.