Habari
China yapewa kipaumbele katika uchimbaji wa chuma nchini

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amefanya mazungumzo na Balozi mpya wa Tanzania katika Jamhuri ya watu wa Chinaj Mhe. Khamis Mussa Omar kwa lengo la kumpitisha kwenye vipaumbele vya Serikali vinavyosimamiwa na wizara hiyo.
Dkt. Abdallah amemwambia Balozi Omar kuwa kwa sasa Serikali inainagalia China kwa jicho la kipekee kutokana na ushirikiano uliopo baina ya mataifa hayo lakini pia kutokana na miradi mbalimbali iliyowekezwa wa makampuni ya China hapa nchini. Akizungumza mara baada ya kikao hicho kilichofanyika Oktoba 08, 2023 Mkoani Dar es salaam,
Dkt. Abdallah amesema, eneo kipaumbele ambalo linahitaji uwekezaji ni eneo la uchimbaji Chuma Liganga na Mchuchuma na mradi wa Chuma wa Maganga matitu. Ameongeza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muumgano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ana dhamira ya dhati ya kukwamua mradi huo na tayari ameshalipa fidia kwa wananchi ili kupisha uwekezaji uweze kuanza. Katibu Mkuu amemtaka Balozi Omar aende nchini China na kuzungumza na wawekezaji wanaoweza kuwekeza kwenye eneo hilona maeneo mengine
Kwa upande wake BaloziOmar amesema, Mbali na eneo la chuma lakini pia ataangazia namna ambavyo China itashirikiana na Serikali ya Tanzani katika kukifufua kiwanda cha Nguo cha Urafiki amabacho kilijengwa kwaa ushirikiano baina ya mataifa hayo mawili