Habari
Chuo cha Elimu ya Biashara CBE kampasi ya Mbeya chashauriwa kuwekeza katika mfumo wa masafa ili kuwezesha vijana wengi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ameuagiza Uongozi wa Chuo cha Elimu ya Biashadra (CBE) kampasi ya Mbeya kuwekeza zaidi katika mifumo ya masafa ili kuwezesha vijana wengi waliko mbali kuchangamkia fursa za kupata elimu y ibiashara ikiwa ni pamoja na kupata fursa zilizopo ndani na nje ya nchi
Dk.Mpango ameyasema hayo leo 31/07/2023 mara baada ya kuzindua Kampasi na Majengo ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Kampasi ya Mbeya. Ameyasema hayo wakati akizungumza na Mamia ya wananchi wa Kata ya Iganzo jijini Mbeya ambao walifika kwa wingi Chuoni kushuhudia tukio hili adhimu la kihistoria.
Alisema ni wakati sasa kwa Wahadhiri wa Chuo cha CBE kwenda na wakati ili kusaidia vijana wanaopata masomo na elimu kutofanya biashara kwa mazoea .
“Viongozi wa Chuo wekeni mipango itakayowesha taasisi hii kutoa elimu bora ya biashara kwa vijana kwa maslai mapana ya Taifa na maendeleo ya nchi yetu. ”alisema.
Aidha Dk Mpango ametumia fursa hiyo kuonya wanafunzi wanaopata fursa ya elimu kuitumia kuanzisha biashara zenye kuleta tija na kuachana na kujiingiza kwenye vitendo vya hanasa katika Jiji la Mbeya.
Alisema Wananchi walio wengi wanafanya biashara kwa mazoea, kupitia uwekezaji huu, niwatake wahadhiri kufikilia kutoa elimu ya mifumo ya masafa ya kibiashara kwa vijana ili kuleta tija ya ushindani wa ndani na nje ya nchi.
Aidha alimueleza Mlezi Chuo hicho, Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson kuwa amesikia ombi lake la miundombinu ya elimu na barabara na kuahidi kulifikisha kwa Mawaziri wenye dhamana.
Kwa Upande wake Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini, alimueleza Makamu wa Rais, eneo la mradi huo lilitolewa na wazee wa Kata ya Iganzo, huku akishukuru Wizara ya viwanda na biashara kwa kuwekeza katika Chuo cha CBE.
Awali Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu kijaji katika Salamu zake akimkaribisha Makamu wa Rais amesema kuwa Wizara Wizara ya Viwanda na Biashara yenye dhamana ya kusimamia Taasisi zote zilizo chini yake kikiwemo Chuo Cha Elimu ya Biashara CBE wameamua kuwekeza Mbeya badala ya kuhudumu huduma zikiwa zinatolewa Dare s Salaam au Dodoma pekee.
Amesema Majengo yaliyozinduliwa yamegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1 na milioni 40 ,ambapo bilioni 1 na milioni 100 zimetoka katika mapato ya ndani ya Chuo na milioni 350 zimetoka kwenye mfuko Mkuu wa Serikali
"Mhe. Makamu wa Rais tunashukuru sana tupelekee shukrani zetu kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuongezea pale tulipokuwa tumeanza,hatime hatua ya kwanza ya kuendeleleza hizi hekali hizi 54 imekamilika",Alisema Dkt Kijaji.