Habari
PONGEZI TANTRADE KWA KUTUANDALIA MAONESHO YENYE HADHI YA KIMATAIFA SABASABA 2025.
PONGEZI TANTRADE KWA KUTUANDALIA MAONESHO YENYE HADHI YA KIMATAIFA SABASABA 2025.
2 JUNI, 2025.
Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Prof Palamagamba Kabudi ameipongeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa kazi nzuri ya uratibu wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwa kuzingatia viwango vya kimataifa sambamba na wakati uliopo. Aidha Waziri Kabudi amepongeza ubunifu uliofanya na washiriki wa Maonesho ya Sabasaba 2025 msimu wa 49 na kutoa wito wa kufanya maandalizi kabambe ya Maonesho yajayo kwa mwaka 2026 ambapo Maonesho ya Sabasaba yakatimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake, ameyasema hayo leo pindi alipotembelea Maonesho ya Sabasaba 2025 yanayofanyika katika kiwanja cha Mwl Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.