Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Dkt.Abdallah Azindua Gari ya ASHOK LEYLAND nchini.


Dkt.Abdallah Azindua Gari ya ASHOK LEYLAND nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah  amesema Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuweka mazingira bora na wezeshi kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi ili waweze kufanyabiashara  kwa urahisi na tija.

Ameyasema hayo Julai 19, 2023 kwa niaba  ya Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji(Mb. ) wakati  akizindua  gari aina ya Ashok Leyland  kutoka India chini ya Kampuni ya usambazaji ya Kifaru Motors iliyopo nchini Tanzania katika ukumbi wa Golden Tulip jijini Dar es Salaam.

Aidha, Dkt. Abdallah  amesema jitahada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan zinawahakikishia wafanyabiashara mazingira wezeshi na usalama wa bidhaa na watu na hivyo kuvutia wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kufanya biashara nchini

Vilevile,  Dkt.Abdallah ameipongeza Kampuni hiyo ya Kifaru Motors kwa kutambulisha gari hiyo ya Ashok Leyland ambayo itasaidia katika usafirishaji wa bidhaa mbalimbali hasa bidhaa au mazao yanayotoka mashambani na vijijini kufika katika masoko kwa urahisi.

Naye,  Balozi wa India nchini Tanzania Mhe.Biyana S. Pradhan amefurahishwa na kutambulishwa kwa gari hiyo mpya nchini Tanzania ambayo itaongeza biashara ya usafirishaji wa bidhaa nchini na Tanzania kuwa sehemu ya soko la magari hayo.

Vilevile, Mkurugenzi wa Kampuni ya Kifaru Motors Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luongo amesema kuwa amefurahishwa na Serikali ya Tanzania kwa kuweka mazingira bora ya ufanyaji biashara hasa kwa wanaofanya biashara wa bidhaa kutoka Nchi za Nje ya Tanzania.