Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Dkt. Abdallah: Serikali itaendelea kuwaenzi kuwalinda na kuwatunza Wawekezaji nchini.


Dkt. Abdallah: Serikali itaendelea kuwaenzi kuwalinda na kuwatunza Wawekezaji nchini.

Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amesema Serikali  ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea  kuwaenzi, kuwalinda na kuwatunza wawekezaji wanowekeza nchini. 

Aidha, ametoa rai kwa Wawekezaji kuendelea kuwekeza kwa kuwa Serikali inaendelea kuweka mazingira bora na wezeshi  pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza kupitia Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Nchini (MKUMBI)

Dkt. Abdallah ameyasema hayo  kwa Juni 24,2023  Mkoani Iringa Wilaya ya Mufindi alipokutana na  kusikiliza changamoto za
Wamiliki wa Viwanda vya kuzalisha bidhaa za mazao ya misitu hususani  Vinia inayotumika kutengeneza bidhaa mbalimbali kama plywood MDF, na marine boards.

Akisikiliza changamoto zao baada ya kutembelea baadhi ya Viwanda vikubwa vinavyozalisha Vinia mpaka zao la mwisho na vidogo vinavyozalisha vinia peke yake, Dkt. Abdallah amesema  Wizara kwa itashirikiana  na Mkoa wa Iringa pamoja na Wakala wa Misitu (TFS )  kutatua changamoto  zote zilizojitokeza ili wawekezaji hao waendelee kuzalisha bidhaa hizo  kwa tija

Naye Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa Bi. Asifiwe Mwakibete    ametoa kwa wawekezaji kuendelea kuwekeza katika viwanda vya mazao ya misitu mkoani humo kwa kuwa  malighafi ya miti inapatikana kwa wingi na wananchi waendelee kupanda miti kwa kuwa soko la miti ya mbao ni kubwa Mkoani humo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga Bw., Ayoub Kambi  amesema kwa kushirikiana na Mkoa wa Iringa wataweka mikakati ya kutatua changamoto zote  zilizojitokeza  kwa wawekezaji wa viwanda vinavyotengeneza bidhaa kwa kutumia Vinia

Vinia ni moja ya mazao ya misitu yanayohandisiwa ( Engeneered Wood Products(EWP) inayotumika kutengeneza moja kwa moja bidhaa za mazao ya mbao. Vilevile  hutumika kutengeneza plywood, marine boards, samani, vifaa vya michezo, makasha ya kusafirisha bidhaa na ujenzi wa majengo na miundombinu mbalimbali.

Wilaya ya Mufindi ina viwanda 27 vinavyoshughulika  na uzalishaji wa vinia. Kati ya hivyo viwanda 6 vinauwezo wa kuzalisha bidhaa hadi hatua ya mwisho kama plywood MDF na marine board  kwa kutumia vinia na viwanda vingine vinaishia  hatua ya malighafi ya vinia.