Habari
.Dkt. Ashatu Kijaji leo tarehe 28 Machi, 2023 amefanya ziara ya Kikazi katika Taasisi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TanTrade

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe.Dkt. Ashatu Kijaji leo tarehe 28 Machi, 2023 amefanya ziara ya Kikazi katika Taasisi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TanTrade) ambapo, amepokea Taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na mradi wa TanTrade App ambao utawasaidia Wafanyabiashara nchini kujua taarifa za biashara na bei za bidhaa kwenye masoko mbalimbali kwa kila siku .
Katika ziara hiyo Mhe. Dkt.Kijaji aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil T. Abdallah na kufanya kikao cha pamoja na Mwenyeki wa Bodi ya Wakurugenzi ya TanTrade Prof. Ulingeta Mbamba na Wajumbe wa Bodi hiyo, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa Khamis na Menejimenti ya TanTrade kwa Ujumla.