Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Dkt. Hashil Abdallah afanya Mazungumzo na Wawekezaji kutoka China.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah amekutana na kufanya mazungumzo na Wageni kutoka Nchini China
ambao wamedhamiria kuanzisha Viwanda vinne hapa Nchini.

Dkt.Hashil amekutana na Wageni hao Agosti 18,2023  katika Ukumbi wa Mikutano wa Mkandarasi Jijini Dodoma na kuwahakikishia ushirikiano Mkubwa wa Kibiashara na Uwekezaji wa Viwanda hivyo Nchini Tanzania.

Viwanda hivyo vinavyotarajiwa kuanzishwa Nchini ni pamoja na Kiwanda cha Mazao hasa mazao ya Mihogo chini ya Bw.William Chu,Kiwanda cha Kutengeneza Pikipiki chini ya Bw.Pan Fauxian,Kiwanda cha Ujenzi wa Nyumba za Kisasa za bei nafuu chini ya Bw.Lyu Sunxiong pamoja Kampuni ya Usafirishaji chini ya Zhang Qingfu.