Habari
KAPINGA: SERIKALI ITAENDELEA KUSAIDIA VIWANDA VYA SARUJI NCHINI.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga amesisitiza kuwa Serikali itandelea kuweka mazingira bora ya ufanyaji biashara na uwekezaji katika viwanda vya saruji, ili kuongeza fursa za ajira na mchango wa kiuchumi wa sekta ya saruji nchini Tanzania.
Ameyasema hayo Machi 17, 2026 wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Saruji ya Dangote nchini Tanzania, Bw. Adeyemi Fajobi Jijini Dodoma.
Kikao hicho, kilichohudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Hiyo, Bw. Aristides Mbwasi, kilijikita katika kujadili mikakati ya kukuza uwekezaji wa viwanda vya saruji vya Dangote vilivyopo Mtwara, Lindi, Dar es Salaam, na Tanga.
Mazungumzo yameangazia namna ya kuongeza uzalishaji, kuvutia uwekezaji zaidi, na kuhakikisha viwanda hivi vinapata malighafi muhimu pamoja na rasilimali nyingine zinazohitajika.
