Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

DKT JAFO ATAKA MAONESHO YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KUWA YA KITAIFA


.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo(Mb) ameagiza kuwa Maonesho ya Biashara na Uwekezaji yanayofanyika kila Mwaka Mkoani Pwani yanakuwa katika ngazi ya Kitaifa kama yalivyo Maonesho mengineyo ya Biashara.

Ameagiza hayo Desemba 17,2024 wakati wa Uzinduzi wa maonyesho hayo ya nne katika Mkoa huo ambayo yameshirikisha wawekezaji mbalimbali pamoja na wajasiriamali wadogo wa Mkoa huo.

Dkt. Jafo pia amesema Serikali inaendelea kuweka Mazingira wezeshi kuvutia wawekezaji hivyo ameziagiza Taasisi wezeshi kutokuwa wakwamishaji kwa wawekezaji hao wanaotaka kuwekeza nchini kwani wakizingatia utoaji huduma wao utachangia kuvutia wawekezaji wengi.

Aidha Dkt.Jafo amewataka wazalishaji wa bidhaa kuzingatia ubora wa bidhaa ambazo zitakidhi kushindanishwa katika masoko ya ndani na nje ya nchi na Kuwataka Watanzania kupenda bidhaa zinazozalishwa nchini ili kusaidia kukuza sekta ya uwekezaji.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe.Abubakar Kunenge amesema kutokana na ongezeko la megawati kwa asilimia 19 limesababisha wawekezaji kufanya shughuli zao za uzalishaji muda wote ukilinganisha na awali ambapo walikuwa wakizaliisha kwa siku tatu hadi nne kwa wiki.