Habari
Dkt. Kijaji akutana na Mkurugenzi Mkuu wa cha A-Z. kilichopo Kisongo Jijini Arusha

Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Ashatu Kijaji (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha A-Z Bw.Kalpesh Shah na Meneja wa Masoko wakiwanda hicho Bw.Slivester. Kazi
Kikao hicho kimefanyika tarehe 25 Mei 2023 katika ofisi ndogo za Mhe Waziri zilizopo katika jengo la PSSSF jijini Dodoma. Aidha pamoja na mambo mengine kikao hicho kilikuwa na lengo la kupokea taarifa za uzalishaji na uendeshaji wa kiwanda hicho kinachozalisha bidhaa za nguo kilichopo Kisongo jijini Arusha.