Habari
Dkt Kijaji ateta na DCO kujenga uwezo wa Biashara Mtandao

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Ashatu Kijaji (Mhe.) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Digital Cooperation Organization (DCO) Bi. Deemah Al Yahya
kuhusu kujengea uwezo Taasisi za Tanzania kwenye masuala ya biashara mtandao Aprili 29, 2024 wakati wa Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani unaloendelea Jijini Riyadh, Saudi Arabia.