Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

erikali ya Tanzania imedhamiria kujenga misingi shindani na endelevu yenye ubora wa utoaji wa huduma wenye kuwezesha biashara nchini


Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdalah amesema Serikali ya Tanzania imedhamiria kujenga misingi shindani na endelevu yenye ubora wa utoaji wa huduma wenye kuwezesha biashara nchini kwa kuzingatia jiografia na rasilimali watu kwa kupitia sera mikakati na mipango shindani na shirikishi.

Amesema hayo wakati wa hafla fupi ya kupokea Cheti cha umahiri wa kutoa huduma ya Ithibati Ubora na bidhaa kutoka SADCAS iliyofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana Disemba 06,2024

Amesema ili kuwa na misingi ya ushindani katika soko la ndani na nje na kuwa na ubora wa Kimataifa na kuweza kushindana sokoni ni lazima kuwa na Mamlaka inayohusika na Viwango yenye mifumo inayoatambulika na kuaminika kimataifa kupitia viwango vya kimataifa na hivyo Serikali inatenga bajeti kila mwaka kuwezesha TBS kuboresha mifumo yake ya udhibiti na ubora.

Aidha amesema cheti hicho kwa TBS ni kuthibitisha na kutafsiri maono na miongozo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan juu ya kuingia kwenye masoko ya kimataifa kwa kuwa na bidhaa bora kwani huo ni uthibitisho kuwa bidhaa inayothibitishwa na TBS inaweza kuuzwa kwenye masoko ya Kimataifa hivyo ni fursa kwa Wafanyabiashara na Wazalishaji kutumia Shirika hilo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma za Ithibati Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADCAS) amesema wanatoa vyeti hivyo kwenye taasisi zinazohusika na viwango kwenye nchi wanachama ili kuonesha ushindani katika bidhaa zinazozalishwa ikiwa ni pamoja na bidhaa za Saruji,Vioodozi, pamoja,Vinywaji na nyinginezo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma za Ithibati za Jumuiya ya maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADCAS) Bi. Eve Christine Gadzikwa amesema kabla ya Cheti hicho cha Umahiri katika Ithibati Ubora,TBS walishapatiwa cheti cha Umahiri katika huduma za Maabara pamoja na cheti katika mifumo ya usimamizi hivyo Shirika hilo linapiga hatua kubwa kwenye Viwango vya ubora.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Dkt. Ashura Katunzi amesema cheti hicho kimethibitisha kuwa huduma zinazotelewa na Shirika hilo ni za Kimataifa hivyo wazalishaji wataweza kupeleka bidhaa zao kwenye masoko ya Kimataifa.