Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Hatua kuwachukuliwa hatua za kisheria kwa wamiliki wa Viwanda na wazalishaji wa bomba (holepipes) wanaokiuka sheria za viwango


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo (Mb) ameliagiza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ifikapo mwezi Desemba,2024 kuwachukulia hatua za kisheria kwa wamiliki wa Viwanda na wazalishaji wa bomba (holepipes) wanaokiuka sheria za viwango vinavyowekwa na Shirika hilo ikiwemo kuteketeza bidhaa hizo na gharama za uteketezaji zitakuwa chini ya mmiliki wa bidhaa hizo.

Amayasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa bodi ya Shirika hilo Septemba 05,2024, katika Ukumbi wa Ofisi za Makao Makuu ya shirika hilo,Dar es Salaam.

Dkt.Jafo ametoa maagizo hayo kutokana na malalamiko yaliyopo kwa wazalishaji hasa wa mabomba (holepipes) kutofuata viwango vilivyowekwa na shirika ambapo bomba moja linatakiwa kuwa na urefu wa mita 6 na unene wa milimita 1 na uwepo wa maelezo ya bidhaa(Mark)

Katika kuhakikisha kuwa Serikali inawalimda Wananchi wake Dkt.Jafo ameliagiza shirika hilo kushirikiana na Ofisi ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa kubaini wazalishaji wa vinywaji vikali ambavyo havifuati viwango cilivyowekwa na shirika hilo ambao ndio chanzo cha vifo vingi kwa Watanzania na kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa watumiaji wa bidhaa hizo nchini.

Aidha Dkt.Jafo amesema kwasasa mchakato wa kanuni ambao utakamilika hivi karibuni ambao utawataka wazalishaji wa bidhaa za chakula wanaongeza virutubisho ili kuondokana na tatizo la udumavu kwa watoto nchini hivyo TBS ina jukumu kubwa la kusimamia hilo

Vilevile Dkt.Jafo amelipongeza Shirika hilo kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya na kuiasa bodi hiyo mpya kuendelea na kazi nzuri zaidi ya pale walipoishia ili kuwa shirika bora kwa manufaa ya nchi.