Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

UWEKEZAJI KIWANDA CHA MAFUTA: DKT. HASHIL AKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA INDIA


Katibu Mkuu wa Wzira ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amekutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya B.L. Agro Industries ya nchini India Bw. Ashish Khandelwal Kuhusu Kampuni hiyo yenye nia ya kuwekeza Kiwanda cha kisasa cha Kusindika Mafuta ya Kula nchini (Edible Oil).

Mazungumzo hayo yamefanyika Agosti 31, 2025 katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es salaam.