Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara kwa Mhandisi Simion Irege Charles amekutana na kufanya mazunguzo na Naibu Makamu wa Rais wa Idara ya Sera na Tathimini


Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara kwa Mhandisi Simion Irege Charles amekutana na kufanya mazunguzo na Naibu Makamu wa Rais wa Idara ya Sera na Tathimini Department of policy and evaluation) Bi Martha Bowen kutoka Washington nchini Marekani.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara zilizopo katika mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma tarehe 15 Novemba 2024.

Akiongea kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Kaimu Katibu Mkuu Mhandisi Charles Ilege amesema kuwa, amafurahishwa na ujio wa ugeni wa Bi.Martha hapa nchini Tanzania

Aidha, ameishukuru Serikali ya Marekani kupitia Idara ya Sera na Tahimini nchini humo kwa kuwa na mpango wenye manufaa makubwa kwa Taifa letu husasani kwenye sekta ya Biashara utakaosaidia kuweka mazingira mazuri ya ufanyaji Biashara na kuondoa vikwanzo mbalimbali visivyo vya kiushuru.

Kwa upande wake Bi Martha Bowen amesema kuwa ujio wake hapa nchini unalengo la kukusanya taarifa mbalimbali ili kuona mradi utakaoanzishwa wenye lengo la kutoa matokeo makubwa katika sekta ya uwekezaji na biashara utakaosaidia kuondoa vikwazo visivyo vya kiushuru ili kuboresha mazingira ya biashara.

Ameongeza kuwa, ukusanyaji taarifa hizo utalinganisha uzoefu uliowahi kupatikana katika miradi ya aina hiyo iliyowahi kuanzishwa huko nyuma hapa nchini.