Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Conrad Milinga ameongoza kikao cha utambulisho wa msimamizi wa mradi mpya wa Kaizen awamu 3 Bw. Adachi Shinya kutoka JICA.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Conrad Milinga ameongoza kikao cha utambulisho wa msimamizi wa mradi mpya wa Kaizen awamu 3 Bw. Adachi Shinya kutoka JICA. 

Kikao hiki kilikuwa na lengo la kupitia sehemu za utekelezaji wa Mradi mpya ambao unajulikana kwa jina la Business Development Service (BDS)  ambapo utatekelezi wake ni wa kipindi cha miaka 4 Kuanzia Juni 2023 hadi 2027.

Mradi utatekelezwa kwenye mikoa 8 ya Tanzania Bara ambayo ni Dodoma, Singida, Arusha, Mwanza, Morogoro,  Mbeya, Dar es Salam na Kilimanjaro na kwa upande wa Visiwani mradi utatekelezwa Unguja.

Mikoa hiyo tayari imeshatekeleza Kaizen kwa awamu mbili zilizopita kwa kuongeza Tija na Ubora katika Uzalishaji.  Hivyo mradi  huu mpya unaenda kuongeza ujuzi katika nyanja za masoko, uhasibu na technolojia katika sekta za uzalishaji na huduma.