Habari
Kamati ya Bunge yaipongeza TEMDO kwa ubunifu wa kutengeneza vifaa tiba
Kamati ya Bunge yaipongeza TEMDO kwa ubunifu wa kutengeneza vifaa tiba
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imeipongeza Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania (TEMDO) kwa ubunifu wa utengenezaji wa mitambo mbalimbali kwa gharama nafuu pamoja na vifaa tiba vinavyookoa fedha nyingi kwa kuagiza vifaa hivyo nje ya nchi.
Vilevile, Kamati hiyo imeitaka TEMDO kuongeza wigo wa utoaji huduma kwa kuanzisha vituo katika kila kanda nchini, kuongeza juhudi katika kujitangaza pamoja na kuendelea kutafuta vyanzo mbadala vya kuongeza mapato ili iweze kutekeleza shughuli zake kwa ufanisi.
Hayo yamesemwa na Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Deodatus Mwanyika ( Mb) wakati wa uwasilishaji wa Taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya TEMDO iliyo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa Kamati hiyo Agosti 15, 2024 katika ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.
Aidha, Wajumbe wa Kamati hiyo walipata fursa ya kutoa maoni na mapendekezo mbalimbali yaliyolenga kuboresha utendaji kazi wa TEMDO ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakubwa kupata huduma na bidhaa kwa urahisi na gharama nafuu.
Naye, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa ameambatana na
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda Bw. Needpeace Wambuya, ameihakikishia Kamati hiyo kuwa Wizara yake itayafanyia kazi maoni na mapendekezo yote yaliyotolewa na kuahidi kushirikiana na Kamati hiyo katika kuiwezesha TEMDO kutejeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Akitoa maelezo kwa Kamati hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Prof. amesema TEMDO imebuni na kutengeneza vifaa tiba vya hospitali na zahanati nchini ikiwemo Vitanda vya Kujifungulia mama wajawazito, Vitanda vya Kulazia Wagonjwa, Makabati ya kuhifadhia vitu vya Wagonjwa, Majokofu ya kuifadhia Maiti, Kiteketezi cha Taka hatarishi zinazo zalishwa na mahosipitali, mtambo wa kukamulia mafuta ya alizeti, mitambo ya bei nafuu ya kuchuja na kusafisha mafuta ya alizeti (sunflower oil mini-refinery plants), mtambo mdogo wa kuchakata sukari, mtambo wa kusindika zabibu na