Habari
Kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda,biashara ,Kilimo na mifugo imeridhishwa na utendaji kazi wa watumishi waliopo katika Mpaka wa Tanzania na Kenya (Horohoro)
Kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda,biashara, Kilimo na mifugo imeridhishwa na utendaji kazi wa watumishi waliopo katika Mpaka wa Tanzania na Kenya (Horohoro) kupelekea kukusanya mapato zaidi ya asilimia 100.
Pongezi hizo zimetolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati Mhe.Mariam Ditopile kwaniaba ya kamati hiyo walipotembelea Mpaka wa Tanzania na Kenya (Horohoro) katika Kituo cha kukusanyia ushuru wa Forodha pamoja na kuona utendaji kazi wa Taasisi za Wizara ya Viwanda na Biashara hususani Tume ya Ushindani (FCC) @fcc_tanzania , Shirika la Viwango Tanzania (TBS) @tbs_viwango na Wakala wa Vipomo Tanzania (WMA) @wakalawavipimotanzania kwa kushirikiana na Taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika mpaka huo.
Aidha Mhe.Ditopile ameagiza Wizara Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha kuhakikisha inaona namna ya kununua Scanner na Forklift ili kuimarisha utendaji kazi wa ukusanyaji ushuru kwenye mpaka huo ili kuongeza tija.
Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Selemani Jafo ameahidi suala la upatikanaji wa nyenzo kufanyiwa kazi huku akipongeza Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoendelea kufanya kwenye nyanja mbalimbali hapa nchini.
Akizungumzia Viwanda vilivyobinagsishwa ambavyo mpaka sasa vimeshindwa kufanya kazi, Mhe.Jafo amesema kwa kushirikiana na hazina Serikali itaangalia namna ya kufanya kutokana na ukweli kwamba serikali ilikuwa na nia nzuri nyakati ilipoamua kuvibinafsisha.