Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YAPOKEA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA


Wizara ya Viwanda na Biashara yawasilisha taarifa ya utekelezaji wa Majikumu kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria leo tarehe 09 Februari, 2022 Bungeni, Dodoma.

Akifungua kikao hicho, Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) amesema kuwa Wizara yake imejipanga kuandaa sera ya Local content itakayosaidia kuondoa changamoto na kutoa fursa kubwa zaidi kwa wawekezaji wazawa katika miradi ya serikali.

Aidha Mhe. Kigahe amesema kuwa Wizara ipo katika hatua za kuanzisha mfumo wa kuunganisha taasisi zote ili kuwa na dirisha moja la kutoa huduma za vibali na leseni kwa wawekezaji kwa njia ya mtandao.

akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Sera na Mipango Bw. James Mganga ameeleza kuwa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara imeendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia miongozo mbalimbali ya kitaifa na Kimataifa ikiwemo Dira ya Taifa ya Maendeleo (TDV) 2025, Mpango wa tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/22-2025/26).

Aidha, Bw. Mganga ameeleza utekelezaji wa Majukumu ya Wizara katika kipindi cha Mwezi Julai hadi Desemba, 2021 ikiwemo uboeshaji wa Mazingira ya Uwekezaji ambapo wizara imeanza mchakato wa mapitio ya sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996 ili iendane na mazingira ya sasa ambayo inatarajiwa kukamilika kabla ya kumalizika kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Ameongeza kwa kusema kuwa Wizara imejipanga katika kuhakikisha inaipa kipaumbele sekta binafsi kushiriki katika miradi na ziara za serikali ambapo hilo limekwishaanza kufanyika kwa sekta binafsi kushiriki katika ziara ya serikali nchini Kenya, Msumbiji na Uganda.

Aidha Mhe. Kigahe amewaahidi waheshimiwa wabunge kufanyia kazi maoni yote yaliyotolewa na wajumbe wa kamati hii. 

Katika kikao hiki cha kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria kilihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil T. Abdallah.