Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya  Viwanda, Biashara, Kilimo na Biashara  yaishauri Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya  Viwanda, Biashara, Kilimo na Biashara  imeishauri Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kuwa na Mipango Mikakati inayolenga kuendeleza sekta ya uwekezaji, viwanda na biashara inayoshabihiana na mikakati inayolenga kuendeleza sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi. 

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. David Mwakiposya Kihenzile (Mb.) wakati  Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ikiwasilisha Taarifa  kuhusu Muundo na majukumu yake kwa Kamati hiyo Machi 12, 2023 katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

Amesema mipango mikakati hiyo pia ilenge kuongeza ajira, kuwa na usalama wa chakula ikiwemo upatikanaji wa sukari na mafuta ya kula ili kupunguza uagizaji wa chakula nje ya nchi, utafutaji wa masoko  ya bidhaa za tanzania ndani na nje ya nchi na usimamizi wa miradi ya kielelezo ili kukuza uchumi wa viwanda. 
 
Nao Wajumbe wa Kamati hiyo walitoa maoni mbalimbali yaliyolenga kuboresha utoaji huduma  na utendaji kazi shirikishi wa sekta hizo fungamanishi za uwekezaji viwanda, biashara, kilimo na mifugo 
uzalishaji wa viwanda vya kuongeza thamani karibu na maeneo mazao hayo yanapolimwa usimamizi wa mabaraza ya uwezeshaji kiuchumi ngazi ya wilaya, kuboresha utoaji wa mikopo kwa wajasiliamali, utoaji wa nembo ya ubora katika bidhaa na usimamizi wa vipimo sahihi katika bidhaa. 

Akijumuisha maoni na mapendekezo ya Kamati hiyo, Naibu Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara  Mhe. Exaud Kigahe amesema Wizara itaendelea kutekeleza kikamilifu ushauri na maelekezo ya Kamati hiyo ili kuboresha utendaji kazi na ushirikiano wa wizara kuboresha utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara nchini

Awali Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwasilisha Taarifa hiyo alisema  Wizara inajukumu kubwa la kuleta maendeleo jumuishi na endelevu kwa kutumia raslimali zilizopo katika sekta ya uwekezaji, viwanda na biashara ili kuchangia kuongeza ajira na kukuza uchumi wa Taifa

Aidha, ameiahidi kuwa Wizara  iko tayari kutoa ushirikiano kwa Kamati hiyo katika kutekeleza jukumu kubwa la Wizara hiyo katika kisimamia utekelezaji wa Sera, Sheria, Mipango, Programu na Mikakati inayoweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi ili kuzalisha bidhaa zinazokidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi, ushindani katika biashara na uwekezaji katika viwanda.