Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo yapokea Taarifa ya Matrekta ya URSUS


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara,Kilimo na Mifugo ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mhe.Mariam Ditopile imepokea na kujadili taarifa ya hatua zilizofikiwa za utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Spika na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo kuhusu Malalamiko ya wakulima juu ya Matrekta ya URSUS kutoka Nchini Poland.  

Taarifa hiyo imewasilishwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Ashatu Kijaji Oktoba 17,2023 Katika Ukumbi wa Bunge Jijini Dodoma.  

Aidha Kwaniaba ya Serikali Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge na Uratibu Mhe.Jenista Mhagama,Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe,Naibu Waziri wa Fedha Mhe.Hamad Chande,Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara Dkt.Hashil Abdallah pamoja na baadhi ya wakuu wa Idara na Taasisi.