Habari
KAPINGA: WANANCHI KAGUENI BIDHAA KABLA YA KUNUNUA
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, ametoa wito kwa wananchi wote kuwa makini kwa kufanya ukaguzi wa kina kabla ya kununua Bidhaa ili kujilinda na madhara ya bidhaa bandia.
Waziri Kapinga Ameyasema hayo Aprili 7, 2026 baada ya Operesheni ya Bidhaa Bandia nchini huku akiwasisitiza Wananchi umuhimu wa kusoma tarehe za uzalishaji na mwisho wa matumizi (expiry date), pamoja na kutumia simu janja kuhakiki alama za usalama kama Barcode na QR Code kupitia mifumo rasmi ya Serikali kama Hakiki ya TRA kWa Bidhaa Bandia no hayati kwa Afya za binadami, hivyo umakini wa mlaji ndio kinga ya kwanza.
Aidha amewahakikishia kuwa Serikali imejipanga kupitia Mpango wa kudhibiti bidhaa hizo sokoni kwa kutumia mifumo ya kidijitali ya ufuatiliaji (Tracing System) unalenga kutambua mnyororo mzima wa bidhaa kuanzia kiwandani hadi kumfikia mlaji wa mwisho ili kuhakikisha usalama wa mtumiaji na Taifa kwa ujumla,
Waziri Kapinga pia amebainisha kuwa udhibiti huu ni sehemu ya mikakati ya Wizara na Taasisi zake kama FCC, TBS, na BRELA kuendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara na kuondoa bidhaa zote zisizo na ubora zilizopo sokoni.
Lengo kuu la jitihada hizi ni kulinda uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla kwa kukuza ushindani wa haki na kulinda mapato ya Serikali.
