Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

KAPINGA AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI WA KIWANDA CHA PIKIPIKI ZA UMEME


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga (Mb) amewakaribisha wawekezaji wa Kampuni ya Plug and Ride Tanzania, katika Kiwanda cha uunganishaji wa magari ya umeme ya miguu mitatu na pikipiki.

Vilevile, amewahakikishia kuwa Serikali inaendelea kuweka mazingira bora na wezeshi kwa ajili ya ukuaji wa sekta hiyo muhimu nchini katika wakati ambao Tanzania inahamasisha matumizi ya nishati safi huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa Kinara wa utunzaji wa Mazingira.

Waziri Kapinga, ameyasema hayo Julai 15, 2026, alivyokutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni Hiyo Bw. Pradeep Chauhan akiwa ameambatana na Bi. Rekha Sharma, katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Wawekezaji hao wa Kiwanda cha Plug and Ride Tanzania wameonesha nia ya kuongeza uwekezaji wao nchini.