Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Katibu Mkuu amesisitiza uwajibikaji


Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amesisitiza uwajibikaji na kujituma katika kutekeleza majukumu ya taasisi na kufanya kazi kwa uweledi na kujiepusha na vitendo vya Rushwa kwani vitendo hivyo havikubaliki.

Dtk. Hashil ameyasema hayo Machi 10, 2023 alipokuwa akizindua Baraza jipya la Wafanyakazi lililofanyika kwenye Ukumbi wa NSSF Ilala Dar es Salaam 

Ameipongeza Wakala wa Vipimo na Uongozi wake kwa kazi nzuri inayofanyika hasa kwa kuingia katika maeneo Mapya ya kazi hasa kwenye eneo la Upimaji wa Dira za Maji na Mita za Umeme.