Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Katibu Mkuu Dkt. Abdallah apokelewa na Wafanyakazi ofisi za Wizara zilizoko Mtumba jijini Dodoma.


Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amepokelewa rasmi na watumishi wa Wizara katika ofisi za Wizara zilizoko Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma na baadae kuongoza kikao cha Menejimenti ya Wizara.

Katika kikao hicho kilichofanyika leo tarehe 27 Desemba, 2022 Dkt. Abdallah ametoa shukrani za pekee kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumteua kuongoza Wizara hii muhimu, Aidha ameongeza kwa kusema kuwa anashukuru sana kwa ushirikiano alioupata kutoka kwa Mhe. Waziri, Naibu waziri, Naibu Katibu Mkuu, Menejimenti ya Wizara na Wafanyakazi wote kwani wao ndio wamekuwa nguzo ya mafanikio yake kiutendaji.

Dkt. Abdallah amewashukuru menejimenti ya Wizara na kuwataka kuendelea kumpa ushirikiano wa karibu katika utekelezaji wa majukumu yake ili kuyafikia malengo ya Wizara katika kuboresha Mazingira ya Biashara Nchini na kuvutia wawekezaji wengi zaidi katika sekta mbalimbali ili kukuza uchumi wa Nchi.

Awali akikabidhi taarifa ya Utekelezaji wa majukumu ya Wizara katika kipindi cha kuanzia tarehe 1 Agosti, 2022, Naibu Katibu Mkuu Bw. Ally Gugu ametoa pongezi za dhati kwa Katibu Mkuu Dkt. Abdallah na kumuhaidi ushirikiano wa karibu katika kutekeleza majukumu ya kazi na kuwa tayari wakati wote kupokea na kutekeleza maelekezo.