Habari
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah afanya mazungumzo na, Makamu wa rais wa Kampuni ya CocaCola

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Ashatu Kijaji amekutana na kufanya mazungumzo na, Makamu wa rais wa Kampuni ya CocaCola anayeshughulikia eneo la Afrika Mashariki na Kati Bi. Debra Mallowah kuhusu fursa za uwekezaji na ufanyaji biashara zilizopo Tanzania.
Mazungumzo hayo yamefanyika wakati wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Marekani na Afrika Mashariki (AMCHAM BUSINESS SUMMIT) linalofanyika nchini Kenya kuanzia tarehe 29-30 Machi, 2023. Pembeni ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe Dkt. John Stephen Simbachewene ambaye pia alishiriki katika mazungumzo hayo.