Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt Hashil Abdallah ametembelea Wakala wa Vipimo Kitengo Cha Bandari


Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt Hashil Abdallah ametembelea Wakala wa Vipimo Kitengo Cha Bandari ili kufahamu shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo Bandarini upande wa Mafuta.

Katika ziara yake ametembelea Bandarini, eneo la  kurasini Oil jet kwenye kituo Cha kushushia mafuta kupitia flow meter na kuona ushushwaji na upimaji wa Mafuta unavyofanyika.

Akiwa kwenye ziara hiyo ameielekeza Wakala wa Vipimo kuendelea kusimamia usahihi wa Vipimo kwenye ushushwaji na usambazwaji wa Mafuta ili kuhakikisha Mafuta yanayopokelewa yapo sahihi kama yalivyoingizwa