Habari
Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amewataka wakufunzi wa KAIZEN nchini Tanzania kuandaa mipango mikakati inayopimika ya utekelezaji wa mradi wa KAIZEN.

Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amewataka wakufunzi wa KAIZEN nchini Tanzania kuandaa mipango mikakati inayopimika ya utekelezaji wa mradi wa KAIZEN.
Dkt. Abdallah ameyasema hayo tarehe 13 Mei, 2023 wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa wakufunzi wa KAIZEN kitaifa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa makumbusho ya Taifa, jijini Dar es salaam.
Dkt. Abdallah ameishukuru Serikali ya Japan kupitia JICA kwa kuleta falsafa ya KAIZEN kwani kwa hapa nchini kwetu imekuwa na mchango mkubwa kwenye sekta ya Viwanda na Uwekezaji inayopelekea ukuaji wa kasi wa Uchumi wa Nchi yetu.
“Mkutano huu wa mwaka wa wakufunzi wa KAIZEN unaunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuweka mazingira wezeshi ya kurahisisha uwekezaji na ufanyaji biashara nchini” Amesema Dkt. Abdallah