Habari
Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hasil Abdallah amesema Serikali ya Tanzania inatambua umuhimu mkubwa wa Metrolojia katika sekta ya afya,

Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hasil Abdallah amesema Serikali ya Tanzania inatambua umuhimu mkubwa wa Metrolojia katika sekta ya afya,
Vilevile amesema Serikali imeendelea kujizatiti kwa kuwekeza katika utafiti wa hali ya juu, kukuza ushirikiano kati ya wataalam wa maabara ya afya na wataalamu wa vipimo na kukuza utamaduni wa usahihi katika utambuzi na matibabu ndani ya nchi yetu na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Dkt. Abdallah ameyasema hayo Juni 19,2023 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Metrolojia wa Kanda ya Afrika Mashariki unaohusu Vipimo kwa Afya uliofanyika Jijini Dar es salaam.
" Afya ni msingi wa jamii yenye ustawi . Maendeleo katika utafiti wa matibabu, mbinu za kisasa za utunzaji wa afya, na usahihi katika utambuzi na matibabu yanatuwezesha kufikia matokeo bora ya afya kwa wote." Amesema Dkt Hashil.
Aidha, amesema kupitia kanuni thabiti za vipimo, tunaweza kulinda usalama wa mgonjwa, kupunguza makosa ya uchunguzi na kuboresha matokeo ya afya kwa wote
Vilevile, Dkt. Abdallah ametoa rai kwa Nchi Wanachama wote kunufaika na huduma zinazotolewa na metrology hususani sekta ya afya
katika nyanja mbalimbali za maisha ya kila siku.