Habari
Katibu Mkuu wizara ya viwanda na biashara, Prof. Riziki Shemdoe apokea ujumbe kutoka COMESA.
Katibu Mkuu wizara ya viwanda na biashara, Prof. Riziki Shemdoe apokea ujumbe kutoka sekretarieti ya soko la pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika COMESA. Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe leo tarehe 27 Februari, 2020 amepokea ujumbe kutoka Sekretarieti ya Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA) ulioongozwa na Balozi Dr.Kipyego Cheluget, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia miradi. Ujumbe huo ulifika katika ofisi za wizara zilizopo katika eneo la Mtumba jijini Dodoma lengo likiwa ni kukutana na Menejimenti ya Wizara kuzungumzia utekelezaji wa mradi unaohusu uwezeshaji biashara (Trade Facilitation) na kuimarisha biashara ya mipakani (Cross Border Trade). Pande zote mbili zimekubaliana kushirikiana kwa karibu zaidi katika utekelezaji wa mradi huo ambao unatarajia kuchochea na kurahisisha biashara kwa nchi wanachama wa Jumuiya za COMESA, EAC na SADC.