Habari
Kongamano la Kimataifa la nchi zinazotekeleza Mradi wa EIF lafanyika tarehe 11 - 13 Septemba, 2023 Geneva, Uswizi .

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa Balozi wa Tanzania nchini Uswizi Mhe. Maimuna Tarish katika picha ya pamoja baada kushiriki
Kongamano la Kimataifa la nchi zinazotekeleza Mradi wa EIF lililofanyika tarehe 11 - 13 Septemba, 2023 Geneva, Uswizi ambapo aliongoza ujumbe wa Tanzania.
Kongamano hilo lililenga kutoa fursa kwa nchi zinazotekeleza mradi wa EIF kubadilishana uzoefu wa utekelezaji wa mradi, uendelevu wa Vitengo vya Kitaifa vya uratibu jumuishi wa biashara, utumiaji wa raslimali na utaalamu wa washirika wa EIF, mabadiliko ya kimfumo yanayochochea kuongeza uwezo wa uzalishaji, ushirikishwaji wa sekta binafsi na thamani ya fedha.