Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Tanzania Kuimarisha Mifumo ya Chakula


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ametaja namna ambavyo Tanzania imedhamiria kufikia lengo namba mbili la umoja wa mataifa (SDG2) linalohusu kuufikia ulimwengu usio na njaa mwaka 2030.

 Akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano la Mifumo ya Chakula (AGRF) lililofanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa (JNICC) Dkt. Mpango amesema Kongamano hilo utainufaisha Tanzania kuimarisha mifumo ya chakula kwa kuwekeza zaidi kwenye rasilimali ardhi na nguvu kazi ya wanawake barani Afrika.

 Amesema Tanzania inajivunia jitihada za maboresho ya mifumo ya chakula na imejitoa kushirikiana na wengine ambapo lengo kuu ni kuwa na ulimwengu usio na njaa ifikapo mwaka 2030.

 Akitoa mifano ya namna Tanzania imeweka jitihada kwenye suala hilo Dkt. Mpango amesema, hivi sasa kilimo hapa nchini kinatambulika kama chanzo kikuu cha ukuaji wa uchumi ambapo kimetoa ajira kwa zaidi ya asilimia 65 ya wananchi huku kikichangia katika pato la Taifa kwa asilimia 27 Tanzania Bara na asilimia 21 kwa Zanzibar.

 Amesema sekta ya kilimo inachangia katika usafirishaji wa bidhaa zake nje ya nchikwa zaidi ya asilimia 30 na kuzalisha asilimia 65 za malighafi kwa ajili ya viwanda vya Tanzania.