Habari
Maonesho ya 24 ya Biashara ya Afrika Mashariki yafunguliwa Diamond Jubilee

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt Ashatu Kijaji (Mhe.) amefungua rasmi Maonesho ya 24 ya Biashara ya Afrika Mashariki Oktoba19, 2023 katika ukumbi wa Daimod Jubeel, jijini Dar es Salaam
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo, Dkt. Kijaji alisema kuwa maonesho hayo yanatoa fursa ya kukuza biashara na uwekezaji nchini Tanzania, kuongeza ajira, kuzalisha bidhaa halisi, na kuvutia uwekezaji kutoka nje ya nchi.
Dkt. Kijaji alieleza kuwa maonesho hayo yanashirikisha makampuni 120 kutoka Tanzania, Afrika Mashariki, Ulaya, na Asia. Makampuni ya Tanzania yanawakilishwa na makampuni 25, huku makampuni ya kigeni yakiwakilishwa na makampuni 95.
Vikevile. amesema yanapokutanishwa makampuni hayo kuja kuonesha bidhaa zao hapa nchini kunaleta fursa ya kuongeza Ajira na kuzipa thamani malighafi zinazozalishwa hapa nchini na kutengeneza bidhaa halisi. Aidha, Aliwataka watanzania kushiriki maonesho hayo kwa wingi ili kujifunza kuhusu bidhaa na huduma zinazopatikana nchini na nje ya nchi.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Biashara Afrika Mashariki Expo group Duncan Njage amewasihi watanzania kuja kujitokeza kuona bidha bora katika maonesho kwani mbali na kuleta fursa yatawapatia ajira ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Maonesho hayo yataendelea kwa siku tatu, kuanzia leo hadi Oktoba 21.
Muhtasari: